Taita Taveta: MCAs wamvua shati Samboja, wabakisha kaptura tu

August 2024 ยท 1 minute read

- Bunge la kaunti hiyo litalazimika kumpa nafasi kujitetea kala ya seneti kujadili kuhusu kutimuliwa kwake

- Kufuatia hatua hiyo, Samboja sasa atasubiri kufahamu hatma yake kwa kuwa ni lazima hoja iliyotumiwa kumtimua kujadiliwa katika Bunge la Seneti

Wawakilishi Wadi wa Kaunti ya Taita Taveta wameamua kumfuta kazi Gavana wao Granton Samboja, kwa wanachodai ni kutumia mamlaka vibaya.

Habari Nyingine: Bobi Wine awashinda ujanja askari wa Museveni, awahepa kwa kuparamia bodaboda

Wakati wa kikao cha kumtimua, Wawakilishi Wadi zaidi ya 25 wanadaiwa kupiga kura na kuidhinisha kutumuliwa kwa gavana wao.

Kufuatia hatua hiyo, Samboja sasa atasubiri kufahamu hatma yake kwa kuwa ni lazima hoja iliyotumiwa kumtimua kujadiliwa katika Bunge la Seneti.

Habari Nyingine: Mpangaji kortini kwa kumhangaisha 'landlady'

Pia bunge la kaunti hiyo litalazimika kumpa nafasi kujitetea kala ya seneti kujadili kuhusu kutimuliwa kwake.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZoVzf5Jmq5qhpJZ6ta3VnquaZZ2YrrR51pqkr62RYsCprdOiZKyZnZe8q62MsJibmZuewKmtjKSYqaylp65uwNRnn62lnA%3D%3D